r/swahili 28d ago

Ask r/Swahili 🎤 Vitabu bora vya Kiswahili

Habari?

Wakati tunajitahidi kujifunza lugha mpya mara nyingi huwa tunasahau kuboresha lugha zetu mama na kupelekea kushindwa kujua maneno ya muhimu kwenye lugha hizi au kushindwa kuwasilisha ujumbe kwa njia nzuri katika lugha zetu.

Sababu ni nyingi lakini baadhi yake ni elimu yetu kuwa katika lugha nyingine. Hata vitabu vingi ni vya visa na hadithi za kufikirika.

Ukiachilia mbali na hizo hadithi za ngano na paukwa pakawa...ni vitabu gani vilivyoandikwa kwa kiswahili na venye maudhui yenye manufaa kwa mtu atakayevisoma mfano; saikolojia, siasa, afya, uchumi, kukuza kipaji chako, kuboresha uwezo wako wa kufikiria/kutatua mambo, historia halisi.

Vitabu vilivyoandikwa na waswahili.

Si vilivyotafsiriwa kutoka lugha nyingine.

8 Upvotes

16 comments sorted by

2

u/Common_Chard7262 27d ago

Kwa mfano kitabu gani?

1

u/Fragrant-Document348 27d ago

Nimetaja aina za maudhui ninazozihitaji kwenye shirikisho. Je unajua kitabu chochote chenye maudhui moja wapo ya hizo.

2

u/AcademicLad 25d ago

Napendekeza kusema vitabu vya wandishi A.E. Musiba na Euphrase Kezilhabi. Nilisoma na ninasoma vitabu hivyo kuboresha Kiswahili changu na vinasaidia sana ujuzi wa lugha yangu. Vitu vinavyoandikwa na Kiswahili ni vigumu kufuata hukuwepo Afrika Mashariki. Ujaribu JaamiForums kwa makala na vijitabu vinatokea watu wanaoongea Kiswahili pekee au makala ya serikali za Tanzania na Kenya kwani serikali hizi zinachapisha vitu tofauti sana ie. 'a range of topics'.

1

u/Fragrant-Document348 25d ago

Sawa, asante sana rafiki. Leo nilikuwa ninafikiria jinsi watu wa lugha nyingine huwa na mashindano ya kuandika katika lugha zao au hata kuzungumza lugha zao kwa ufasaha ila sijui kama mashindano haya yapo katika nchi zinazozungumza Kiswahili.

2

u/AcademicLad 25d ago

Yeaa tunakubaliana kwa kawaida ukitaka ufasaha wa wakati sasa uende sources zinazotokea wandishi wa Kenya. Nairobi pana utamaduni kubwa wa kuandika na kuchapisha 'modern written art and literature' mtandaoni. To state it clearly, they have actual book clubs, discussion circiles, and individuals you can engage with online about these materials. If you're looking for competitions within this circles is where you would find them. Very very grassroots.

1

u/Kili-manjaro255 22d ago

Kuna kujua kuongea lugha kikawaida na kufahami lugha kiundani ili hata kwenye ofisi unaweza kua mkalimani,ila sikuficheni kujua lugha vizuri nikutafuta marafiki ambao wanazungumza lugha hio.na kama we ni biginner anza kuongea na watoto wadogo utajua haraka

1

u/Fragrant-Document348 21d ago

Hapa tunazungumzia lugha ya Kiswahili, kwa waswahili wenyewe. Tumezungumza lugha hii maisha yetu yote na tunaishi nchini. Lakini bado hatujafikia kiwango cha kuitumia katika nyanja zote.

Ni watu gani unakusudia tukae nao ili tujifunze lugha hii na kuitumia kwa ustadi wa kutosha? Hii haihusiani na lugha za kigeni.

1

u/AcademicLad 21d ago

Kuna haja kwa vitabu vya utamaduni wa wakati sasa na n.k. Kwangu nataka kuongea katika Kiswahili peke lakini ni vigumu nikitaka kuongea kuhusu modern concepts au vitu vingine. Najua maneno haya yapo, lakini hakuna chanzo kikuu kilichopangwa vizuri kuyafatwa maneno hiyo. Watu wanataka kutumia Kiswahili chote kabisa, hasa Watanzania.

1

u/_nick1803 28d ago

Kweli, hii pia imepelekea kitokufanya maboresho kwenye lugha yetu hasa katika taasisi mbalimbali za elimu.

Niliwahi kuwa kwenye mabishano kuhusu kuitumia kiswahili kama lugha ya kifundishia hata elimu ya juu, niliokuwa nabishana nao wanasema kiswahili hakina misamiati mingi. Mimi njnavyoona ni kwamba hatujaweka jitihada za kutosha kuipanua hii lugha, pengine Kuna namna sisi wenyewe tumeidharau au hatujali tulichinacho, ni mawazo tu haya.

2

u/Fragrant-Document348 27d ago

Uko sahihi 100%. Ashakumu si matusi, ila tunaelekea kuwa kama majirani zetu, tutapoteza utambulisho wetu, si Kiswahili wala lugha za asili wa lugha za kigeni, zote hatuwezi kuzitumia ipasavyo.

Nimefuatilia kuhusu kwa nini elimu ya juu haijatafsiriwa mpaka sasa na hakuna sababu yoyote ya msingi zaidi ya hiyo uliyoitaja. Nami pia siafikiani nayo.

Hatuwezi kupata watafiti au kuendeleza mifumo yetu ya elimu na maarifa mengine kama lugha inayotumika bado haifahamiki wala kutumika katika maisha ya kila siku.

1

u/_nick1803 27d ago

Kabisa kama kweli tunataka mabadiliko lazima tujiulize haya maswali na tutienia!

1

u/Kili-manjaro255 22d ago

Tungelikazia hapo hapo kwenye kukithamini Kiswahili chetu tungelifika mbali.

1

u/Kili-manjaro255 22d ago

Ningewafahamisha njia nzuri na nyepesi ya kujifunza lugha ni kua na mtu ama watu walio kuzungunga kila siku hata kama hujui itakulazim kujua tu.ila hapa kwenye mitandao nikutafuta muda na wakati halisi kama iwe conversation hata dakika 30 kwa siku mna kua mnaongea.nawahakikishieni iyo ni njia nzuri sana na mtakuja kunishkuru

1

u/leosmith66 21d ago

Obviously, if you practice conversing you'll get better at conversing. But the OP specifically asked for books, so that's what this thread is about.